Monday, November 16, 2009

STREET DJ 2009 DSM, YAFIKA UKINGONI


Hawa ndio ma Dj walioingia ktk tano bora, hapa wakijitambulisha kabla ya kuanza kwa shindano lililofanyika Jollys Club siku ya tarehe 14 Nov 2009, jumamosi

Washiriki wakiwa na Muwakilishi wa Serengeti breweries (Dada queen) pamoja na Jaji kiongozi (Mwenye karatasi mkononi)

he he he Wenyeji wa Jolly nao hawakuwa mbali kutaka 'snap' na 'winner' wa street Dj kama unavyowaona wakim'tite' Dj bora wa kitaa 2009 (Si walijua kuna mkwanja hapo)

Mshindi wa Kwanza-Ally Mustapha

Mshindi wa pili James Zacharia akipokea zawadi

Mshindi wa tatu Machumu Makongoro akipokea zawadi

Mshindi wa nne Innocent Willard akipokea zawadi yake

Sunday, November 15, 2009


Mshindi wa tano-Alex Ashery Akionesha zawadi yake ya mkwanja alopokea


Mandojo na Domo Kaya wakipagawisha


RaHa RAha rAhA--- Serengeti hazikuwa mbali kila Dj aliondoka na katuni moja

My wife. ohhh sory, Mke wa Mkurugenzi wa MIL Investment akimuangalia mzee kwa makini.

FURAHA!!! Dj atakaebahatika kushinda leo hapa, zawadi atakayoipata nitaizidisha mara mbili, ndiyo ahadi aliyotoa Mkurugenzi wa MILL Investment.
Mgeni wa heshima, Mkurugenzi wa MIL Investment PEDESHE Ndama kama wengi wanavyomwita akikaribishwa na mtangazaji wa C2C TV Ray mshana, kutoa machache alokuwa nayo kuhusiana na shindano la kumtafuta Dj Bora wa mtaa (Street Dj)


Mshiriki no 1 -James Zacharia akifanya majamboz hata kisigino kiliruhusiwa nini kichwa,alikuwa ana manjonjo si ya kawaida kila aliyemuona alifurahishwa na mbwembwe zake.

Mshiriki no.2 akitoa burudani kwa makiiiiini huku akiwaangalia kama kuna shabiki atasogea katika stage,yaonekana anaijua kazi yake, na ni kweli kila alipokuwa anabadilisha nyimbo watu wanaongezeka

Mshiriki no.3, Machumu Makongoro akimwaga njonjo zake kwa kusugua sugua

Mshiriki no.4 Alex Ashery akiwahakikishiwa mashabiki waliofika jollys kama yeye ni mkali

Mshiriki No.5-Innocent Willard,Dj aliyekuwa na furaha na kutabasam muda woooote, yaonekana hata kama angesitishwa ushiriki wake siku hiyo ya fainali,sidhani kama sura yake ya tabasam ingebadilika (SAFI SANA KIJANA)

Hivi ndibyo ilivyokuwa stage ya Jollys kabla ya shughuli yoooote ya kumtafuta dj bora wa mtaani
Marketing Executive (Queeen) Akitoa nasaha zake za busara kwa vijana wanaochipukia katika fani ya U-Dj

Uwiiiiiiii, hapa uvumilivu zero, aliekunwa na nyimbo za dj hakuweza kuvumilia,ahhhh unajikuta upo kati mwanangu

Tuesday, November 10, 2009

STREET DJ SASA FAINALI

Lile shindano lililokuwa likisubiriwa na wengi la kumtafuta Dj bora wa kitaa mkoa wa D'salaam lililoandaliwa na 3G entertainment na QSSP Group linafika ukingoni.
Fainali inatarajiwa kufanyika katika club ya jolly's iliyopo maeneo ya Upanga, siku ya Jumamosi tarehe 14/11/2009 kuanzia saa 3 usiku.Fainali hizi ilikuwa zifanyike katika Club ya Maisha kwa bahati mbaya club hiyo imepata tatizo kubwa la kuungua moto ambalo kutatuliwa kwake hakuna anaejua lini utakuwa tayari.Uongozi wa 3G unatoa pole kwa mkasa mzima uliotokea Club Maisha

Monday, November 9, 2009

MAISHA CLUB YAUNGUA



Hivi ndivyo maisha club ilivyoteketea kwa moto pichani ni Kiota kilichokuwa kikitumiwa na Maisha Club kikiwa kimeungua kabisa

Tuesday, September 8, 2009

Street Dj Yaingia kitaa kwa kitaa,yafanyika mtaa wa Ruponda magomeni Makuti nyuma ya kanisa la Katoliki


Ma-dj wa kitaa wakisubiri kwa hamu shindano lililofanyika katika viwanja vya magomeni makuti mtaa wa Ruponda,nyuma ya kanisa Catholic



mipigo hii je????kila mmoja alionyesha manjonjo yake hakuna aliekubali kuonekana hajui

Majaji waalikwa wakimsifu dj na kumtoa kasoro yake

Mkurugenzi wa 3G na majaji waalikwa wakichagua nani mkali atakaeendelea katika shindano

Wadau wa shindano wakibadilishana mawazo

Hata sisi tunataka kuwa madj wa kitaa

Thursday, August 27, 2009

Shindano ya kumtafuta balozi wa kiswahili kanda ya kinondoni yamefanyika vatican hotel na washindi na washiriki hawa hapa,jionee vimwana wa '"kiswaz"


washindi wa3 wa shindano la kumtafuta balozi wa kiswahili,katikati ndio mshindi wa kwanza na wa pili kulia ni mshindi wa 3, aliebaki ni mshindi namba 3



Wachezaji wa Twanga pepeta wakikamua nao walikuwepo!!!


watatu!!!!!mh sijui macho ndo yalimfanya ashinde?????

mshindi wa pili katika kinyang'anyiro hicho

mshindi wa kwanza wa mashindano ya kumtafuta balozi wa kiswahili

Mshindi wa kwanza na wa pili katika smile la kuwaaga washabiki

Nani mzuri kunizidi? mrembo akionekana kama anajiuliza

Kweli mrembo  wa kiswahili !!!

Kimasa je?

Kazi kubwa walioifanya majaji hawa ni kama ulivyoiona hapo