Tuesday, November 10, 2009

STREET DJ SASA FAINALI

Lile shindano lililokuwa likisubiriwa na wengi la kumtafuta Dj bora wa kitaa mkoa wa D'salaam lililoandaliwa na 3G entertainment na QSSP Group linafika ukingoni.
Fainali inatarajiwa kufanyika katika club ya jolly's iliyopo maeneo ya Upanga, siku ya Jumamosi tarehe 14/11/2009 kuanzia saa 3 usiku.Fainali hizi ilikuwa zifanyike katika Club ya Maisha kwa bahati mbaya club hiyo imepata tatizo kubwa la kuungua moto ambalo kutatuliwa kwake hakuna anaejua lini utakuwa tayari.Uongozi wa 3G unatoa pole kwa mkasa mzima uliotokea Club Maisha