My wife. ohhh sory, Mke wa Mkurugenzi wa MIL Investment akimuangalia mzee kwa makini.
FURAHA!!! Dj atakaebahatika kushinda leo hapa, zawadi atakayoipata nitaizidisha mara mbili, ndiyo ahadi aliyotoa Mkurugenzi wa MILL Investment.
Mgeni wa heshima, Mkurugenzi wa MIL Investment PEDESHE Ndama kama wengi wanavyomwita akikaribishwa na mtangazaji wa C2C TV Ray mshana, kutoa machache alokuwa nayo kuhusiana na shindano la kumtafuta Dj Bora wa mtaa (Street Dj)
Mshiriki no 1 -James Zacharia akifanya majamboz hata kisigino kiliruhusiwa nini kichwa,alikuwa ana manjonjo si ya kawaida kila aliyemuona alifurahishwa na mbwembwe zake.
Mshiriki no.2 akitoa burudani kwa makiiiiini huku akiwaangalia kama kuna shabiki atasogea katika stage,yaonekana anaijua kazi yake, na ni kweli kila alipokuwa anabadilisha nyimbo watu wanaongezeka
Mshiriki no.3, Machumu Makongoro akimwaga njonjo zake kwa kusugua sugua
Mshiriki no.4 Alex Ashery akiwahakikishiwa mashabiki waliofika jollys kama yeye ni mkali
Mshiriki No.5-Innocent Willard,Dj aliyekuwa na furaha na kutabasam muda woooote, yaonekana hata kama angesitishwa ushiriki wake siku hiyo ya fainali,sidhani kama sura yake ya tabasam ingebadilika (SAFI SANA KIJANA)